Chanzo Cha Ugomvi wa Nandy na MWijaku hiki hapa,Wamedhurumiana Hela.

Mambo yamezidi kuwa ya moto baada ya Mwijaku kuvujisha sauti ya Nandy akidaiwa kuwa alikuwa akimtuma akamchafue mwanadada superstaa kutoka lebo ya Wasafi,Zuchu.

RELATED : Vita ya Nandy na Zuchu imefikia pabaya, Nani Mchokozi?

Vyanzo mbalimbali vimeripoti kuwa chanzo cha Mwijaku kuvujisha mazungumzo hayo ni kile kinachodaiwa kuwa hakupata haki yake ya malipo kutoka kwa Nandy.Kutokana na Sauti nyingine ya Nandy iliyovuja inasemekana kuwa Mwijaku alimpa Nandy namba ya mtu ambaye angeweza kumsaidia kupata udhamini kwenye tamasha lake huku akitegemea pengine angepata mgawo wa asilimia kadhaa kutoka kwenye ili hilo ambapo mpaka sasa imeonekana kuna dalili kuwa za Nandy kumzima Mwijaku au kumpa asilimia chache tofauti na matarajio yake kwa hiyo Mwijaku akaamua kumwaga Ugali.

Kwenye baadhi ya Sauti na Screenshot za mazungumzo kati ya Nandy na MWijaku inaonekana kuwa Mwijaku alikuwa anatarajia kupata anagalau milioni kumi kutoka kwenye mgawo huo bila kugawa na mtu yeyote ambapo inaonekana kuwa Nandy alikuwa tayari kumpatia milioni tatu tu jambo lilimkasilisha Mwijaku na kuamua kuvujisha sauti ya mazungumzo yao ili kumharibia Nandy.

Japo ambalo amelifanya Mwijaku ni kama kumnunulia Nandy maadui ambao bila shaka wengi wao watakuwa ni mashabiki wa WCB na wote wanaompenda Zuchu kwani picha inayotengenezwa ni kwamba Nandy anamwonea wivu Zuchu.

Also, check more tracks from Nandy;

Leave a Comment