Sijiskii Vibaya Kufananishwa na Vanessa Mdee – Saraphina

Mwimbaji wa Bongo fleva anayekuja kwa kasi Saraphina amedai kuwa hajisikii vibaya pale watu wanamfananisha au kusema kuwa anamuiga Vanessa Mdee.

Katika Mahojiano yake na moja ya media Saraphina amefunguka na kusema watu wengi ni kama wanamshambulia kuwa kuna namna anafanana na Vanessa Mdee lakini yeye anadai kuwa haijawai kumpa shida ukilinganisha na status ya Vanessa kwenye tasnia ya Muziki.

“Mimi sijawahi kujisikia vibaya kwa vanessa ni msanii ambaye amekwepo kwenye industry kwa muda mrefu na amefanya vitu vikubwa na vijana wengi wanamuangalia kama role model,kwa hiyo mtu akinifanisha naye kwangu ni sifa”,alisema Saraphina.

Leave a Comment